Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Issa Q'asim, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain, ameelezea kufanya uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni kuwa ni usaliti mkubwa zaidi na ni kujisalimisha kwa mradi wa “Israili Kubwa”.
Ametahadharisha kuwa kufanya uhusiano wa kawaida ni “msaada wa moja kwa moja kwa adui” na ushiriki katika jitihada zake za “kuuvunja Umma”.
Ayatullah Issa Q'asim amesisitiza kuwa; kufanya uhusiano wa kawaida na adui wa Kizayuni – iwe kwa dhahiri au kwa siri – si kujisalimisha mapema tu, bali ni zaidi ya hapo, ni msaada wa kweli kwa adui na ushiriki wa dhati katika jitihada zake za kuuvunja Umma.
Katika taarifa aliyotoa tarehe 5 Septemba 2025, ameutaja hili kuwa ni usaliti mbaya zaidi katika safu ya kufanya uhusiano wa kawaida, na ni kujitenga na Umma, dini na thamani zake, iwe katika ngazi ya vitendo au kwa misingi ya undugu, ghayra (wivu wa kidini), heshima na hadhi.
Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain ameweka wazi kwamba tamko rasmi la Waziri Mkuu wa Israili, Netanyahu, pamoja na vita vyake vya chuki na vya kiuvamizi vilivyoshirikiana na mkakati wa kidhulma wa Marekani, kwa uwazi kabisa vimeelekeza ujumbe kwa Umma wa Kiarabu na Kiislamu kuhusu kuingia chini ya ubabe wa Israili, iwe kwa njia ya amani au kwa njia ya vita, katika mfumo wanaouita “Israili Kubwa”. Bali hata zaidi, katika fremu pana zaidi inayoyahusisha mataifa yote mawili, kama ambavyo matamanio yao mabaya na yaliyoporomoka yanavyoonesha.
Ayatullah Issa Q'asim amefafanua kuwa vita hivi tayari vimeanza, na vitisho vyake vikubwa vinahusu kila kipande cha ardhi za Kiarabu na Kiislamu na kila kiongozi mwaminifu na mwenye ushawishi wa mataifa haya mawili.
Amehitimisha taarifa yake kwa maneno haya:
“Mwenyezi Mungu auongoze Umma wite na kuufanya umoja katika njia ya Jihadi ya kuzuia uvamizi dhidi yake, dini yake, ardhi yake na maslahi yake, na Mwenyezi Mungu autunuku heshima na ushindi wa wazi.”
Maoni yako